10. Bwana anakuja

1 Bwana anakuja twendeni kumlaki
Bwana Mungu wa majeshi,
Iwasheni mioyo tukampokee
Huyo mwenye utukufu

Refrain:
Karibu Bwana, njoo
Karibu Bwana, njoo
Shinda pamoja nasi.

2 Wewe ndiwe Mfalme,
Mfalme wa mbinguni
Utulishe wenye njaa.
Wewe ndiwe mwanga,
sisi tu vipofu
Tufanye tuone tena. [Refrain]

3 Wewe ndiwe njia,
tutakufuata
Turudi kwa Baba yetu.
Wewe ndiwe, utuangazie
Tusije tukapotoka. [Refrain]

4 Hosana, Hosana,
huyo mbarikiwa
Anakuja kwetu sisi.
Aja kutulisha na kutugawia
Matunda ya ukombozi. [Refrain]

Text Information
First Line: Bwana ankuja twendeni kumlaki
Title: Bwana anakuja
Author: Moses O. M. Mdegella
Refrain First Line: Karibu Bwana, njoo
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Yesu anangojewa
Notes: Asili ya wimbo: Kingoni, Tumshangilie Mungu
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us