Text: | Bwana wetu umetoa |
Author: | C. Vischer |
1 Bwana wetu umetoa
mara moja msalabani
mwili na maisha yako
kwa wokovu mtakatifu.
2 Ndiye kafara ya kweli
itoshayo siku zote;
kima chake ni kikubwa
hakiwezi kuzidishwa.
3 Mbinguni atuombea
akiwa kitini pake.
Na hapa atubariki,
tukila karamu yake.
4 Twaonyesha kufa kwake
mpaka atakaporudi;
tunaungana na yeye
kuwa viungo vyake tu.
Text Information | |
---|---|
First Line: | Bwana wetu umetoa |
Title: | Bwana wetu umetoa |
German Title: | Wir danken dir, Herr Jesu Christ |
Author: | C. Vischer (1600) |
Language: | Swahili |
Publication Date: | 1988 |
Topic: | Chakula cha Bwana |
Notes: | Sauti: Herr Jesu Christ, wahr Mensch und Gott, Asili: Leipzig 1625, Posaunen Buch, Erster Band #20, Nyimbo za Kikristo #140 |