211. Bwana twakuomba sasa

1 Bwana twakuomba sasa:
Tutokee sisi hapa,
kwani siku yako leo.
Tupe, kufikiri vema
neno lako la uzima,
na la ukombozi wetu.
Sisi tuliopotea
tupate kurudi kwako.

2 Yawe mbali kwetu sasa
kila mambo masumbufu.
Roho na mioyo yetu
ikaongee na Mungu.
Tupate kutiwa hamu
ya raha iliyo kwako,
itakayotutokea
baada ya maisha haya.

3 Naona kitini pako
taji lao washindao;
nasikia nyimbo zao
waishao kupigana.
Hao wakusifu wewe
kwa zaburi na kwa shangwe.
Hata mimi nijalie
nipate kufika kule.

4 Upungufu wangu wote
ufunike wewe Bwana;
niwe mtakatifu wako
duniani hapa chini,
nisikose kuingia
furahani kwa wageni,
uliowaita wewe
kuimba nyimbo za shangwe.

Text Information
First Line: Bwana twakuomba sasa
Title: Bwana twakuomba sasa
German Title: Zeige dich uns ohne Hülle
Author: F. G. Klopstock, 1724-1803
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Kumtambikia Mungu: Nyimbo za asubuhi
Notes: Sauti: Zeige dich uns ohne Hülle, Posaunen Buch, Erster Band #57
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us