Text: | Naomba, Bwana ukae nami |
Author: | H. F. Lyte, 1739-1847 |
1 Naomba, Bwana ukae nami,
ukija usiku sasa hivi.
Lakini kwako twaona mwanga,
ukae na mimi, jua bora.
2 Upesi kabisa siku zetu
zitapita, raha hatuoni.
Uharibifu uko popote,
ukae nami, umshinde mwovu.
3 Sitamwogopa tena Shetani,
ukiwa nami unibariki.
Sina mwingine ila wewe tu,
ukae nami hata usiku.
4 Ukae na mimi nikilala,
ukae na mimi nikiamka.
Unisikie Ee, Bwana Yesu,
Ukae na mimi mpaka mwisho.
Text Information | |
---|---|
First Line: | Naomba, Bwana ukae nami |
Title: | Naomba, Bwana ukae nami |
English Title: | Abide with me |
Author: | H. F. Lyte, 1739-1847 |
Language: | Swahili |
Publication Date: | 1988 |
Topic: | Kumtambikia Mungu: Nyimbo za Jioni |
Notes: | Sauti: Eventide by H. W. Monk, 1823-1889, Hymnal Companion #6, Nyimbo za Kikristo #177 |