25. Mungu ni wa utukufu

1 Mungu ni wa utukufu
panapo mbinguni juu,
na kwao wampendezao
duniani raha kuu.
Sikieni nchi zote
huko mjini Betlehemu:
Kristo amezaliwa,
Bwana wetu daima,
Kristo amezaliwa,
Bwana wetu daima.

2 Watu na malaika wote
wanamtukuza Yesu,
ashukaye toka mbingu
kuwa kama maskini.
Akaacha enzi yake,
akavaa unyenyekevu
Kristo amezaliwa,
Bwana wetu daima,
Kristo amezaliwa,
Bwana wetu daima.

3 Asifiwe Mwana Mungu
na Mwokozi wa watu,
mleta mwanga na uzima
Yesu mshinda kuzimu,
mfalme wa utengemano
huko mjini Betlehemu.
Kristo amezaliwa,
Bwana wetu daima,
Kristo amezaliwa,
Bwana wetu daima.

Text Information
First Line: Mungu ni wa utukufu
Title: Mungu ni wa utukufu
English Title: Hark! The herald angels sing
Author: Ch. Wesley (1739)
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Kuzaliwa kwa Yesu
Notes: Sauti: Imechukuliwa kwa Catnate "Gott ist Licht" by F. Mendelssohn, 1840, Tumwimbie Bwana #15, Nyimbo za Kikristo #23, Lutheran Book of Worship #60
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us