33. Niende na wachungaji

1 Niende na wachungaji
nimtazame mponya wangu,
kazaliwa duniani
kwa kunipenda mimi.

2 Nimwimbie na malaika,
niusifu utukufu.
Anautengemaza,
kila moyo umpende.

2 Nikawaze na Maria
jambo hili la ajabu:
Aacha mwili mzuri,
achukua wa kimtu.

4 Nimpelekee vipaji
na watambuzi wa nyota,
na nimpe mali yangu,
hata uzima nimpe.

5 Nakupenda, u Mwokozi,
nikumbuke siku hii.
Uje mwangu moyoni,
uufanye kikao.

Text Information
First Line: Niende na wachungaji
Title: Niende na wachungaji
German Title: Mit den Hirten will ich geben
Author: E. Quandt, 1835-1911
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Notes: Sauti na wimbo: Mit den Hirten will ich geben by A. Rische, 1819-1906, Grosse Missionsharfe, Erste Band #39, Nyimbo za Kikristo #3
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us