Text: | Vumilia utaona mwisho |
Author: | Mch. Sila Msangi |
1 Vumilia utaona mwisho
Kwamba umefika
Kimebaki kitambo kidog
Tufike mbinguni.
Refrain:
Pokea wokovu
Ngao yako imani
Nenda kwake
Yesu Mwokozi;
Pokea wokovu
Ngao yako imani
Nenda kwake
Yesu Mwokozi
2 Kwa imani tutakwenda mbele
Bila kulegea.
Wokovu ni wa thamani kubwa
Kwa damu ya Yesu. [Refrain]
3 Wasikia sauti yasema
Amini Injili,
Ukiwa katika giza kubwa
Amini Injili. [Refrain]
4 Imani kwa mambo yaliyopo
Na yale yajayo,
Mbele yetu ni njia ya kweli
Injili ya Yesu. [Refrain]
Text Information | |
---|---|
First Line: | Vumilia utaona mwisho |
Title: | Vumilia utaona mwisho |
Author: | Mch. Sila Msangi |
Refrain First Line: | Pokea wokovu |
Language: | Swahili |
Publication Date: | 1988 |
Topic: | Kushika mwenendo wa Kikristo: Kumngojea Mungu siku za shida |