69. Twende vitani

1 Twende vitani vitakatifu,
zitakapokuja shida na taabu.
Ngurumo zivume kutia woga.
Mwiteni Mwokozi!
Yesu ni mwanga.

2 Ingawa giza lawafunika,
na raha yenu ikizimika,
na nguvu za mwovu hazina mpaka.
Mwiteni Mwokozi!
Yesu ni mwanga.

3 Shetani aje, akijaribu
kuvunja kazi na kuharibu
hila zake zote na zitakwisha.
Mwiteni Mwokozi!
Yesu ni mwanga.

Text Information
First Line: Twende vitani
Title: Twende vitani
German Title: Zieht fröhlich hinaus
Author: C. G. Bath, 1799-1862
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Epifania, Mission
Notes: Sauti: O worship the King (HANOVER) by W. Croft, London 1708, Posaunen Buch, Erster Band #293, Reichs Lieder #538, Lutheran Book of Worship #548
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us