Text: | Mikononi mwa mitume |
Author: | Mch. Sila Msangi |
1 Mikononi mwa mitume
Kazi ilifanywa,
Si nguvu yao
Walipewa msaada, ndiye Roho,
Wakapata kuona upya tena.
Refrain:
Nenda, nenda
(Kazini tu siache kuyasema)
Sisi ni badala yao.
Mitume wa zamani
Tupe vipawa vya kazi,
Tuifanya kazi yako
Tuifanye kazi yako,
Ututume, ututme, ututume.
2 Tuombe kupata Roho
Tuende kazini.
Si nguvu yetu
Kwa kufanya kazi hii njemo meno,
Tutakwenda haraka kuifanya. [Refrain]
3 Vuvia roho Mtakata
Ndani mioyoni
Utuhuishe
Tupe moto wa Roho, tusimame
Tuwe tayari kwenda, kutumika. {Refrain]
Text Information | |
---|---|
First Line: | Mikononi mwa mitume |
Title: | Mikononi mwa mitume |
Author: | Mch. Sila Msangi |
Refrain First Line: | Nenda, nenda |
Language: | Swahili |
Publication Date: | 1988 |
Topic: | Epifania, Mission |
Notes: | Suati: Mch. Sila Msangi |