14. Mungu Ndiye Mwamba Wetu

1 Mungu ndiye Mwamba wetu, nguvu za milele;
Hatuogopi kwa kuwa twapatana naye.

Refrain:
Kabla ya kuumba vyote dunia na vitu,
Wewe, Mungu, ulikuwa Mungu wa milele.

2 Wewe hutumainiwa zamani na leo.
Nguvu zako zawatosha watu wako, Bwana. [Refrain]

3 Kwako, Wewe miaka elfu ni kama kitambo,
Mbingu zijapotoweka, Wewe utadumu. [Refrain]

4 Mungu ndiye Mwamba wetu, nguvu za milele,
Twakunyenyekea Wewe, Twakutumaini [Refrain]

Text Information
First Line: Mungu ndiye Mwamba wetu
Title: Mungu Ndiye Mwamba Wetu
Refrain First Line: Kabla ya kuumba vyote dunia na vitu
Language: Swahili
Publication Date: 1994
Scripture:
Topic: Irada, Sifa Na Injil
Notes: Sauti (Tune): By David Makathimo (© 1994 by David Makathimo) or ST. ANNE by William Croft (Baptist Hymnal 1991 #74, Redemption Songs #47, Nyimbo za Sifa #10) (Tune 1: Mlio wa G, Mapigo 4/4, Tune 2: Mlio in C, Mapito 4/4)
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us