2. Baba, Mwana Roho

1 Baba, Mwana, Roho, Mungu mwenye enzi,
Kila tukiamka tunakuabudu.
Baba, Mwana, Roho, Mungu wa mapenzi,
Ewe Utatu, tunakusifu.

2 Baba, Mwana, Roho, wakuaminio,
Wanakutolea shukurani zao.
Wakusujudia malaika nao:
Wewe U mwanzo, nawe U mwisho.

3 Baba, Mwana, Roho, sisi tu gizani,
Utukufu wako makosa hauna,
U Mtakatifu, nawe U mapenzi,
U peke yako, mwenzio huna.

4 Baba, Mwana, Roho, Mungu mwenye enzi,
Ulivyoviumba vyote vyakusifu:
Baba, Mwana, Roho, Mungu wa mapenzi,
Ewe Utatu, tunakusifu.

Text Information
First Line: Baba, Mwana, Roho, Mungu mwenye enzi
Title: Baba, Mwana Roho
Original Language: English
Language: Swahili
Publication Date: 1994
Scripture:
Topic: Irada, Sifa Na Injil
Notes: Sauti: Holy, Holy, Holy (Nicaea), Baptist Hymnal 1991 #2, Redemption Songs, #25, Nyimbo za Sifa, #6; Mlio wa D - Mapigo 4\4
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us