Author: N. Hermann, karibu 1480-1561 Appears in 1 hymnal Lyrics: 1 Msifuni Mungu, Wakristo,
aliyetukuka,
atufungulia mbingu
kumtoa mwanawe,
kumtoa mwanawe.
2 Atokaye kifuani
pa Mungu Babaye,
alal sasa Mtoto
mtupu maskini,
mtupu, maskini.
3 Anyonya kwa mama yake,
maziwa chakula,
kwa kweli anatulisha
chakula cha mbingu,
chakula cha mbingu.
4 Ageuza hali yake,
avaa mwili wetu,
na sisi anatuvika
uzima wa Mungu,
uzima wa Mungu.
5 Akawa mtumwa, na mimi
naitwa kibwana,
niwe nduguye na mtoto
wake Mungu Baba,
wake Mungu Baba. Topics: Kuzaliwa kwa Yesu
Msifuni Mungu, Wakristo