Author: John Newton, 1725-1807 Hymnal: Mwimbieni Bwana #51 (1988) Lyrics: 1 Jina lake Yesu tamu;
Tukilisikia
Hutupoza, tena hamu
Hutuondolea.
2 Roho iliyoumia
Kwalo hutibika,
Chakula, njaani pia;
Raha, tukichoka.
3 Jina hili ni msingi,
Ngao, ngome, mwamba,
Kwa hili napata wingi
Kwangu ni akiba.
4 Yesu, Mchunga, Rafiki,
Mwalimu, Kuhani,
Mwanzo, Mwisho, Njia, Haki,
Uzima kifoni.
5 Moyo wangu hauwezi
Kukusifu kweli,
Ila sifa zangu hizi,
Bwana zikubali.
6 Na utakaponiita,
Kuja kwako Bwana,
Huko kwako sitaacha
Kukusifu sana. Topics: Mwaka Mpya Languages: Swahili
Jina lake Yesu tamu