1 Mtini Mponya alipowambwa,
ndipo nimwombapo upozi,
akaniokoa mpenzi.
Mwana wa Mungu,
Mwana wa Mungu!
Mwokozi wangu,
Mtini mponya alipowambwa,
Mwana wa Mungu!
2 Chini ya mti wenye uchungu,
ndipo nimwombapo usafi,
mara kwa damu kaniosha
Mwana wa Mungu.
Mwana wa Mungu!
Mwokozi wangu,
Mtini mpponya alipowambwa,
Mwana wa Mungu!
3 Akaniondolea manza,
ameingia ndani mwangu,
kwani mtini amenifia.
Mwana wa Mungu.
Mwana wa Mungu!
Mwokozi wangu,
Mtini mpponya alipowambwa,
Mwana wa Mungu!
4 Ziwa la damu ya koasi,
linatosa makosa yote,
laniendesha wokovuni.
Mwana wa Mungu.
Mwana wa Mungu!
Mwokozi wangu,
Mtini mpponya alipowambwa,
Mwana wa Mungu!
5 Hicho kijito chenye mali!
U tayari kuzama humo?
Humo utaona uzima!
Mwana wa Mungu.
Mwana wa Mungu!
Mwokozi wangu,
Mtini mpponya alipowambwa,
Mwana wa Mungu!
Source: Mwimbieni Bwana: msifuni Mungu, mfalme wa mbingu na nchi! #89