1 Tuombee Wakristo
duniani,
Wasiache ahadi
za imani.
Refrain:
Ee Bwana,
Utujaze Roho Wako;
Ee Bwana,
Utujaze mioyoni.
2 Tuombee wakuu
wa Kanisa,
Wanaolitangaza
Neno lako. [Refrain]
3 Hata na watawala
wetu wote,
Ili tuzidi kuwa
na amani. [Refrain]
4 Ee Bwana, uwe nao
mataifa,
Wakubali Injili
ya wokovu. [Refrain]
5 Tuwaombee wote
waje Kwako,
Wapate kukusifu
siku zote. [Refrain]
Source: Nyimbo Za Imani Yetu #210