229. Mwezi umechipuka

1 Mwezi umechipuka
na nyota zamulika
mbinguni popote.
Makonde yote kimya,
na kunako mabonde
ukungu mzuri unakaa.

2 Dunia imekuwa
nchi ya utulivu,
ni nyumba ya raha.
Viumbe vyenye taabu,
waume, wake, wana
na watulie usiku.

3 Tukiwa na kiburi,
tu wakosaji sana,
wapuzi kabisa.
Twatunga vya uongo,
na maarifa yote
yametutenga na Mungu.

4 Utuonyeshe, Mungu,
wokovu wa kikweli,
tusijidanganye!
Tukae duniani
kama watoto wema
wamtegemeao Baba.

5 Na sasa ndugu zangu,
tuende kujilaza
kwa jina la Mungu.
Atupe usingizi
sisi tuliochoka,
hata majirani wote!

Text Information
First Line: Mwezi umechipuka
Title: Mwezi umechipuka
German Title: Der Mond ist aufgegangen
Author: M. Claudius, 1740-1815
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Kumtambikia Mungu: Nyimbo za Jioni
Notes: Sauti: Der Mond ist aufgegangen by J. A. P. Schulz, 1767-1800, Nyimbo za Kikristo #181, Tumwimbie Bwana #32
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us