227. Jua limekuchwa

1 Jua limekuchwa,
waja usiku,
tunakaa na Yesu
rohoni mwetu.

2 Nyota zatokea,
ndege watua,
kazi imekwisha,
mwili walala.

3 Bwana ukumbuke
wakuitao,
ukawatulize
na waumwao.

4 Ndoto za wototo
zitoke kwako,
tukifumba macho,
utubariki!

5 Wasafiri bara
na baharini,
linda, wazuie
na wakosaji!

6 Hata asubui
tunapoamka,
upendezwe nasi,
tukikushika.

Text Information
First Line: Jua limekuchwa
Title: Jua limekuchwa
German Title: Abend wird es winder
Author: H. Hoffmann v. Fallersleben (1837)
Language: Swahili
Publication Date: 1988
Topic: Kumtambikia Mungu: Nyimbo za Jioni
Notes: Sauti: Abend wird es wieder by C. H. Rink, 1846, Tumwimbie Bwana #19, Grosse Missionsharfe, Erster Band #24
Tune Information
(No tune information)



Suggestions or corrections? Contact us